Ticker

6/recent/ticker-posts

TFF YATOA SIKU 14 KWA KLABU ZA LIGI KUU NA DARAJA LA KWANZA KUWASILISHA MIKATABA YA MAKOCHA

Na.Boniface Wambura,pamoja na Herman Kihwili.IMEWEKWA SEPT. 19,2013 SAA 6:44 MCHANA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja
la Kwanza (FDL) kuwasilisha mikataba ya makocha wao.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia Septemba 17 mwaka huu.

Kwa klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.

Post a Comment

0 Comments