Ticker

6/recent/ticker-posts

SUNDERLAND 1 ARSENAL 3 RAMSEY APIGA MAWILI,OZIL WE ACHA TU

 Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 14,2013 SAA 3:00 USIKU
Mesut Ozil alicheza mechi yake ya kwanza ya Arsenal baada ya kuchukuliwa kwa ada ya uhamisho ya   £ 42.5million kutoka Real Madrid 
Kikosi cha Kocha wa timu ya Sunderland  Paolo Di Canio leo kilikuwa kikitafuta mpira kwa tochi katika mchezo iliopigwa katika
dimba la timu hiyo Stadium of Light,kwa kushuhudia timu hiyo ikibuluzwa kwa kuchapwa na Arsenal kwa mabao 3 kwa 1.
Aaron Ramsey alishinda mara mbili katika dakika ya 67 na dakika ya 76
Alikuwa ni   Aaron Ramsey aliyeipatia Arsenal mabao 2 katika dakika ya 67 na dakika ya 76 kabla ya kipindi cha kwanza Olivier Giroud kuipatia Arsenal bao la kwanza katika dakika ya 11.
Bao la Sunderland liliwekwa nyavuni na Craig Gardner kwa mkwaji wa penalti.
  Olivier Giroud (kulia) aliyeiwezesha timu yake kuongoza  mbele dhidi ya Sunderlandkabla ya Sunderland kusawazisha
Craig Gardner akiisawazishia   Sunderland kwa mkwaju wa adhabu na kufanya timu hiyo kusawazisha kabla ya arsenal kuwaelemea kwa mashambulizi

Craig Gardner akisheherekea mkwaju wa  adhabu,baada ya kuisawazishia  Sunderland
Aaron Ramsey akishinda bao lake la  pili
Mesut Ozil (kulia) akifurahia pamoja na Giroud baada ya kucheza mechi yake ya  kwanza kwa Arsenal
Siku Mbaya  katika ofisi:Bosi wa  Sunderland Paolo Di Canio aliketi juu ya bango baada ya kuona hali ni mbaya kwa timu yake

Kikosi cha Sunderland (4-2-4): Westwood 7; Celustka 6, Diakite 5, Roberge 6, Colback 6; Vaughan 5 (Gardner 46, 8) Ki 6; Johnson 7, Fletcher 6 (Wickham 77), Altidore 6, Mavrias 5 (Borini 72, 6).
Akiba wasio tumika: Brown, Larsson, Cuellar, Mannone.
Mfungaji: Gardner 48 (pen)
Kadi ya njano: Gardner.
Kikosi cha Arsenal (4-2-3-1): Szczesny 6; Jenkinson 7, Sagna 6, Koscielny 7, Gibbs 7; Flamini 7, Wilshere 7; Ozil 9 (Vermaelen 80), Ramsey 8, Walcott 6 (Monreal 88); Giroud 7 (Akpon 90+3).
Akiba wasiotumika : Frimpong, Miyaichi, Akpon, Gnabry, Fabianski. Booked: Flamini, Sagna.
wafungaji: Giroud 11, Ramsey 67, 76.
Refarii: Martin Atkinson 5
Waliohudhulia: 39.055


Post a Comment

0 Comments