Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 17,2013 SAA 9:28 USIKU
Unajua nini,hii inaitwa kun’gata huku na huku,jamii na michezo inasema hivyo kwa sababu mchezaji wa zamani wa timu ya
Liverpool Jonjo Shelve,ameweza kuleta mchango wa mabao yote 4 yaliyopatikana katika mchezo wa ligi kuu England kati ya Swansea City na Liverpool mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2 kwa 2.
Liverpool Jonjo Shelve,ameweza kuleta mchango wa mabao yote 4 yaliyopatikana katika mchezo wa ligi kuu England kati ya Swansea City na Liverpool mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2 kwa 2.
![]() |
Goli la mapema zaidi:Shelvey akapiga bao la mapema katika dakika ya pili tu na kuiwezesha Swans kuongoza .
|
![]() |
| Samahani lakini:aliwaomba Msamaha mashabiki wa timu yake ya zamani ya Liverpool baada ya kufunga bao la kwanza |
![]() |
Kujikaza kisabuni:"Nilijitahidi kuficha hisia zangu kwa kuwa nawaheshimu mashabiki wa Liverpool"Jonjo aliimbia Sky Sport.
|
![]() |
Amenipa mwenyeweee: Daniel Sturridge akiisawazishia Liverpool baada ya kupewa pasi ya kimakosa na Jonjo Shelvey
|
![]() |
| Kama anastua kijoti vile:Daniel Sturridge akishangilia baada ya kuisawazishia bao timu yake |
![]() |
Nami nimo: Mchezaji wa Chelsea aliyetolewa kwa mkopo kwenda Liverpool Victor Musa alishinda bao la pili ndani ya dakika ya 37 katika mechi yake ya kwanza kwa Liverpool
|
![]() |
![]() |
|
Alikubali: Michu alikwenda moja kwa moja kwa Jonjo Shelvey (kulia) baada ya kuipatia Swansea bao la pili
|
![]() |
Kazi nzuri: Michu akishangilia baada ya kuwasawazishia Swansea bao la pili
|
![]() |
Marafiki wa zamani: Brendan Rodgers (kulia) akisalimiana na meneja wa sasa wa Swansea Michael Laudrup
|
Lakini mara baada ya mchezo Jonjo Shelve amewaomba radhi mashabiki wa timu yake ya Swansea City kwa kuwapa zawadi ya mabao mawili timu yake iyo zamani katika mchezo huo uliopingwa katika uwanja wa uhuru (Liberty Stadium)
"Nataka kusema samahani kwa mashabiki wa Swansea kwa makosa mawili mabaya niliyofanya kwani mimi ni muaminifu,nimewapa zawadi Liverpool na kuweza kutoa sare,nadhani sisi tulistahili zaidi ya wao,nimeumia sana,lakini huu ndio mpira"aliiambia Sky Sport.
Lakini pia Jonjo aliongeza kwa kusema kuwa"si kweli kwamba nilitaka kushangilia(baada ya bao) kwa sababu ni wazi kuwa zamani nilikuwa nikicheza katika klabu ya Liverpool na kuwa na heshima kwa mashabiki,lakini nilijitahidi kuficha hisia zangu",
Kwa maana hiyo sasa, Sare hiyo imeifanya Liverpool ipae hadi kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 10, Arsenal wanafuatia wakiwa na pointi 9.
Kwa maana hiyo sasa, Sare hiyo imeifanya Liverpool ipae hadi kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 10, Arsenal wanafuatia wakiwa na pointi 9.












0 Comments