Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 15,2013 SAA 10:50 JIONI
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo imekubali kuongeza mkataba mpya kwa mujibu wa Klabu hiyo kutoka nchini Hispania.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno,ambaye amekuwa
anahusishwa na kuamia katika klabu ya Machester United Ameongeza mkataba wake hadi Juni 2018.![]() |
| Wote tabasamu: Ronaldo akiwa pamoja rais wa Real Madrid Florentino Perez na wanachama wengine wa Real Madrid |
Vyombo vya habari vya Kihispania vimeripoti mchezaji huyo menye umri wa miaka 28 atakuwa analipwa mshahara kila mwaka wa euro 17m (£ 14.25m).
"Manchester
United ni zamani, Real Madrid ni nyumbani kwangu kwa sasa," alisema
katika mkutano wa vyombo vya habari siku ya Jumapili .
Mkataba mpya unakuja baada ya kuwasili kwa Gareth Bale ambaye uhamisho wake ni rekodi ya dunia kutoka Tottenham mapema mwezi huu kwa kitita cha euro 100m (£ 85.3m).
Ronaldo, ambaye alijiunga na Real Madrid kutoka kwa mabingwa wa ligi kuu nchini England Manchester United mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho ya £80m,na amefunga mabao 203 katika michezo mingi akiwa na Los Blancos(Real Madrid)
![]() |
| Mambo poa: Cristiano Ronaldo akiwa na rais klabu Florentino Perez baada ya sherehe ya kutangaza mkataba wake mpya ndani ya katika Santiago Bernabeu |



0 Comments