Wizara elimu
na mafuzo ya ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa amekutana na wadau wa elimu nchini
katika uzinduzi wa mpango wa (matokeo makubwa sasa) katika sekta ya elimu.
Akizungumza
katika uzindizi huo waziri kawambwa amesema kuwa wizara ya ufundi na mafunzo ya
elimu inayo mipango endelevu ya kuinua,kuimarisha na kuendeleza sekta ya
elimu.Akielezea akielezea mafanikio
katika sekta hiyo waziri kawambwa amesema kuwa,wizara hiyo imefanikiwa katika
mchakato wa kuongeza elimu ya shule za msingi,sekondali na elimu ya ualimu.
Dkt. Shukuru Kawambwa:wizara ina mipango endelevu ya kuinua elimmu nchi.
Aidha
kawambwa ameelezea changamoto katika sekta hiyo ni pamoja na msongamano wa
wanafunzi darasani,katika baadhi ya shule za mijini,upungufu wa vifaa vya
kufundishia na kujifunzia,na ongezeko la watu wasiojua kusoma na kuandika
kufikia 31% kwa mwaka 2010.
Pia
ameelezea mpango huo wa (matokeo makubwa
sasa ),wazili kawambwa ameeleza kuwa ni pamoja na serikali kuamua kutumia
mpango huo katika kutekeleza majukumu ya utendaji kazi wa kiwango cha juu
katika nafasi aliyonayo.


0 Comments