Kwa masikitiko makubwa Blog ya Jamii na Michezo,inatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki kwa kifo cha aliyekuwa mtangazaji Wapo redio Fm katika wa kipindi cha JAMII NA MICHEZO,ambacho kwa sasa kinaitwa DURU ZA MICHEZO,Gracemo Bambanza,aliyefariki usiku wa leo jumatano,majira ya saa 7 usiku.
Akizungumza na Jamii na Michezo,ndugu wa karibu wa Bambanza,ndugu Joseph Mwangomola,amesema Gracemo Bambanza alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda wa miezi inayokadiliwa kuwa ni 4,na ugonjwa huo ndio umesababisha kifo chake,
Aidha Joseph Mwangomola ameongeza kuwa,Shughuli za mazishi bado zinaendelea nyumbani kwake kimara kona,na mipango ya mazishi bado inafanywai,ambapo anatarajiwa kusafirishwa kwenda Karagwe kijijini kwao kwa ajili ya mazishi.
marehemu Gracemo Bambanza
Pia Mwangomola,amesema marehemu Gracemo Bambaza,alikuwa ni kijana wake wa karibu kwani alikuwa wanasari wote katika kanisa la Sinza la EAGT,na kusema amesikitika kwa kuwa Gracemo Bambaza,alikuwa kijana mtulivu na mwenye nidhamu,na kuongeza amejisikia vibaya sana lakini hana la kufanya kwa sababu yeye ametangulia na sisi tutafuata kwani kifo kimeumbwa kwa watu wote.
Naye aliyekuwa mmoja wa watu aliyewahi kufanya nao kazi katika kituo cha redio cha Wapo radio Fm,Mispa Masisi,amesema amesikitika sana kwa sababu alikuwa ni mmoja wa watu walioanzisha kipindi cha michezo katika radio hiyo,na hata acha kumkumbuka kwa kuwa amempa pengo jingine katika kipindi hiko cha DURU ZA MICHEZO baada ya kuondokewa na mtangazaji mwingine mnamo mwaka jana,Marehemu Joseph Mapunda.
Marehemu Joseph Mapunda ni wa pili kutoka kushoto,aliyevaa Flana la brue:(TUTA KUKUMBUKA SANA)
Blog ya Jamii na Michezo inasema kuwa,Bwana alitoa na Bwana alitwaa,jina lake liimidiwe,Ameni
.
Tutazidi kuwapa taharifa za msiba huo kadili tutakapozipata.



0 Comments