Shirikisho la soka nchini Tanzania limetuma maombi kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba kuutumia uwanja
huo kwenye mchezo wa kesho Jumamosi Januari 28, mwaka huu kati Simba na Azam utapigwa kwenye uwanja huo wa Taifa, Dar es Salaam kadhalika keshokutwa katika mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Mwadui ya Shinyanga.
Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaonesha kuwa ligi hiyo huko Mbeya kutakuwa na ‘derby’ kwa maana ya mchezo wa upinzani baina ya timu zinazotoka mkoa mmoja wa Mbeya ambazo ni Tanzania Prisons na Mbeya City utakaochezwa na Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Keshokutwa Jumapili Januari 29, mwaka huu kutakuwa na mchezo mwingine ambao Young Africans itacheza na Mwadui jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Majimaji ya Songea itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Jumatatu Januari 30, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
0 Comments