Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.31,2016 SAA 01:51 JIONI
Baba wa
aliyekua bondia mashuhuri Thomas Mashali, (Malifedha Christopher Mashali)
ameelezea hisia zake baada
ya kupokea taarifa za kifo cha mwanawe ambacho
kilitokea usiku wa kuamkia hii leo jijini Dar es salaam.
Malifedha
Christopher Mashali amesema kwa mara ya mwisho aliwasiliana na mwanawe jana
mchana alipokua kwenye mkutano wa wadau wangumi za kulipwa uliofanyika kwenye
ukumbi wa Sterio Bar uliopo Tandika jijini humo.
Amesema
kwa hakika kifo cha mwanawe kimemuumiza kama mzazi, lakini yaliyobaki kwa sasa
anamuachia mwenyezi mungu.Malifedha
Christopher Mashali pia amekanusha zilizozagaa kuwa mwanaye amebadili dini na kuwa Muislamu na kuitwa Mohammed,lakini mzee
Malifedha Christopher Mashali amesema kuwa yeye taarifa hizo hana,na anatambua kuwa Thomas Mashali ni mkristo na atazikwa kikristo siku ya Jumatano.
Malifedha Christopher Mashali amesema kuwa yeye taarifa hizo hana,na anatambua kuwa Thomas Mashali ni mkristo na atazikwa kikristo siku ya Jumatano.
Hata hivyo
baba wa Thomas Mashari akaeleza kwa ufupi historia ya mwanawe katika upande wa
mchezo wa masumbawi ambao bado alikua anauthamini na kuupenda mpaka alipofikwa
naumauti hapo jana.
Naye mdogo
wa marehemu anayeitwa Chareles Christopher Mashari ambaye pia ni bondia amezungumza
na kipindi hiki na kueleza namna alivyopokea taarifa za msiba wa kaka yake.
SIKILIZA HAPA
0 Comments