FIFA imethibitisha kuwa Sepp Blatter atatembelea Marekani kuhudhuria mashindano CONCACAF Gold Cup mwezi ujao .
Blatter alichaguliwa kwa muhula wa tano kama rais wa FIFA wiki iliyopita, siku mbili tu baada ya maafisa saba wa FIFA na washirika kukamatwa kwa shutuma za kupokea Hongo.
Benki mbili kuu nchini Uingereza Barclays Standard Chartered, na HSBC, zimetajwa katika ripoti ya idara ya ujasusi ya Marekani FBI kuwa zilitumika kufanikisha malipo ya kiinua mgongo na rushwa kwa maafisa wakuu katika FIFA na zinafanyiwa uchunguzi.
Blatter, ambaye hajawahi kukutwa na mashitaka,alidai kuwa mgogoro wa rushwa ulitengenezwa kumn'goa madarakani , na amesisitiza yeye ni mtu haki, wa kuongoza FIFA.
Kabla ya matukio ya wiki iliyopita Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 alikanusha kuwa alikuwa ameepuka kwenda nchini Marekani, huku kukiwa na taarifa za uchunguzi wa FBI kwa viongozi wa zamani CONCACAF(Shirikisho la Amerika ya Kaskazini, ya Kati na Chama cha Soka cha Caribbean ).
Hata hivyo,imebainika kuwa Blatter ana mipango ya kuhudhuria mashindano ambayo yanaanza Julai 7 huko Dallas. FIFA imethibitisha kwamba Sepp Blatter anakusudia kusafiri kwenda Marekani mwezi ujao kwa ajili ya CONCACAF Gold Cup,
Wakati huo huo FIFA,pia imethibitisha katibu mkuu Jerome Valcke atakosa siku ya Jumamosi katika ufunguzi Kombe la Dunia la FIFA kwa wa wanawake nchini Canada .
Mapema Jumatatu, FIFA ilimsimamishwa katibu mkuu wa CONCACAF Enrique Sanz na maafisa wawili wa Kongo kuacha kufanya shughuli yoyote inayohusiana na mpira wa miguu. Rais CONCACAF Jeffrey Webb na msaidizi wake Costas Takkas walikuwa miongoni mwa viongozi wa saba waliokamatwa nchini Uswisi wiki iliyopita.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments