Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.
Katika kundi (A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20,Red Coast,Sifa UTD,Shababi,Ukonga UTD,Zakhem,Ugimbi, Beirahotspurs na Pan Africa.
Katika kundi (B) litakuwa na timu za Yanga U20,Stakishari,FFU,New Kunduchi,Sinza Stars,Changanyikeni,Tuamoyo, Sifapilitan na Azania Unga.
Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,imeingia katika hatua ya pili,ambayo itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali ,ambapo kwa upande wa kundi (A)
Simba U20 vs Red Coast (Karume)
Sifa UTD vs Shababi (Mwl/Nyerere)
Ukonga UTD vs Zakhem (Airwing)
Ugimbi vs Beirahospurs (Bandari)
KATIKA KUNDI (B) Februari 12
Yanga U20 vs Stakishari (Karume)
FFU vs New Kunduchi (Benjamini Mkapa)
Sinza Stars vs Changanyikeni (Kines)
Tuamoyo vs Sifapolitan (Bandari)
Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali,mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani,kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji .
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments