Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa Stars tayari kimewasili Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa maandalizi ya mechi
dhidi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
Mechi hiyo itafanyika Jumapili (Novemba 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Swaziland. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji wote walioitwa na Kocha Mart Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia.
Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.
Wakati huo huo, kikosi cha maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo itachezwa Desemba 9 mwaka huu nchini Tanzania.
Kikosi cha maboresho cha Taifa Stars kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 kitakuwa kinakutana mara moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya mazoezi na kucheza mechi moja ya kirafiki.
Kocha Mart Nooij atatangaza kikosi kwa ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara atakaporejea kutoka Swaziland.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments