Ticker

6/recent/ticker-posts

SOMA ALICHOKISEMA WENGER KUHUSU JACK WILSHERE PAMOJA NA MCHEZO WA LEO

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.NOV.03,2014 SAA 01:23 USIKU

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amebainisha kwamba Jack Wilshere hatakuwepo katika kikosi cha leo Jumanne
cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Anderlecht.

Kiungo huyo wa England, ambaye amekosa mechi mbili za  mwisho kutokana na tatizo la goti, amekuwa mgonjwa katika siku za hivi karibuni na hakushiriki katika mazoezi ya Arsenal siku ya Jumatatu asubuhi, ingawa anatarajiwa kurudi siku ya Jumapili katika Ligi Kuu watakapowafuata Swansea.

Wenger hana wasiwasi na majeruhi kufuatia ushindi wa mabao 3-0 nyumbani siku ya Jumamosi dhidi ya Burnley na ameteua kikosi bila kufanya mabadiliko katika mchezo wao wa kundi D utakaopigwa katika dimba la Emirates.

"Jack amekuwa mgonjwa na hatashiriki. kikosi sawa kama tulivyocheza dhidi ya Burnley, "alisema Wenger.
"Kama tuna nafasi (ya kufudhu), labda, lakini inategemea na matokeo katika mchezo mwingine," aliongeza Wenger.

"Lakini bila shaka sisi tunacheza nyumbani na tuna nafasi ya kushinda mchezo na tunataka kuchukua fursa hii. tuko katika nafasi nzuri na tunataka kutumia faida hii vizuri.
"tunawaheshima Anderlecht kwa sababu wao walionesha mchezo mgumu na kidogo tulishinda kimiujiza, kwa sababu tunahitaji kwenda mpaka dakika ya mwisho. Lakini ni kwamba tutakuwa na ubora wetu katika mchezo huu".
"Tumonya. Tumejifunza mengi kutoka mchezo wa kwanza, na bila shaka, sasa katika uwanja wa Emirates tunataka kushinda mchezo tena. "

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo ) 

Post a Comment

0 Comments