Neil Warnock: hajaridhishwa na utendaji wa refa Phil Dowd |
Neil Warnock amebaki na mshangao kwa maafisa wa mechi kwa kushindwa kufanya 'maamuzi magumu' kwa Crystal
Palace wakati timu hiyo ilipofungwa mabao 3-1 na Sunderland usiku wa kuamkia hii leo.
Ilikuwa ni sekunde chini ya 30 mchezo baada ya kuanza katika uwanja wa Selhurst Park wakati mchezaji wa Sunderland Santiago Vergini alipoonekana kumchezea vibaya Fraizer Campbell ndani ya boksi wakati akikikimbilia kufunga,lakini Palace walinyimwa adhabu.
Warnock anaamini kuwa, siku hizi mara nyingi maamuzi yanakwenda kinyume na timu yake , na amebainisha kuwa Palace hawana matokeo mazuri kwa michezo inayochezwa siku ya Jumatatu kwa mara nyingi.
Akiongea na Sky Sports baadaye na alianza kwa kutafakari juu ya tukio la kunyimwa penalti ndani ya dakika za ufunguzi.
Santiago Vergini (kushoto) alionekana kumchezea vibaya Fraizer Campbell ndani ya sekunde 25 ,lakini Palace walinyimwa penalty. |
Warnock alisema: "Nadhani kila mtu anajua ni penalti. mwamuzi hakuweza kuona, lakini yeye alikuwa katika nafasi kubwa".
"Tulihitaji bahati kidogo katika dakika. nafasi ya pekee sisi tungepewa penalti, ni mtu angeokota mpira na kuutupa kwa mwamuzi - hiyo ingekuwa nafasi ya pekee ya sisi kupewa".
"ilikatisha tamaa sana wakati tukicheza vizuri. Jinsi tumekuwa tukipoteza michezo,mimi milele najua".
"Lakini nalifikiri sisi tulikuwa bora usiku wa leo. Hawakuweza kutoa nafasi yoyote zaidi, vijana hawa. Walikuwa na kipaji usiku wa leo".alisema Neil Warnock
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo )
0 Comments