Msemaji wa klabu Yanga, Baraka Kizuguto |
Baadhi
ya wanachama wa klabu ya yanga wameshindwa kujitokeza katika mchakato
ambao ulioandaliwa na mwenyekiti wa klabu hiyo
Yusuph Manji kujiandikisha
Kama wanapinga makubaliano ya mkutano mkuu ya kumuongezea muda wa mwaka
mzima wa kukaa madarakani.
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa klabu hiyo Baraka Kizuguto
amesema mpaka siku ya ijumaa jioni hakuna aliyejitokeza zaidi ya
mwenyekiti yusuph Manji mwenyewe ambaye alitangaza kwamba yeye atakuwa
wa kwanza kujiandikisha.
"Hakuna mwanachama hata mmoja zaidi ya mwenyekiti Yusuph manji,kwa iyo leo hii tunasema mjadala umefungwa,na hatutazungumzia tena swala hili na tunaelekeza nguvu zetu kwenye maandalizi ya Ligi kuu".
Klabu yanga iliweka Daftari kwa ajili ya kuwapa fursa wale wanaopinga maamuzi ya mkutano mkuu waweze kujiandikisha kama wanakataa maamuzi ya kumuongezea muda wa mwaka mmoja Manji, na Walitakiwa wanachama 1522,lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza, na
ukimtoa Manji basi wanabaki wanachama1521 ambao hawajajitokeza kwa ajili
ya zoezi hilo la kujiandikisha.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments