Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS:KAMATI YA UCHAGUZI YA SIMBA YAMUONDOA TENA WAMBURA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI,NA KUPELEKA RASMI MASWALA YA MAADILI FIFA

 Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.Jun. 16,2014 SAA 06:25 MCHANA
Damasi Ndumbalo akizungumza hii leo
Kamati ya uchaguzi ya simba Imemuandoa kwa mara nyingine tena katika kinyanganyiro cha uchaguzi Michael Richard Wambura.

Akizungummaza na waandishi wa habari muda mchache uliopita
mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba wakili Dk.Damasi Ndumbalo amesema wamemuondoa Wambura kwa sababu amevunja abara ya 6 (1) (a) – (g); 6 (1) (L) na 14(3) ya Kanuni za uchaguzi za TFF – 2013, kwa kufanya kampeni kabla ya muda wake.

"Tuliwapa onyo mara ya kwanza Evans Aveva,Jamuhuri Kihwelo pamoja na Michael Wambura kwa kukiuka maadili kwa kufanya kampeni lakini Michael Wambura alirudia tena mara baada ya kamati ya Rufaa ya Tff kumrudisha katika kinyanga'nyiro"alisema Damasi Ndumbalo 

Katika swala lingine kamati hiyo ya uchaguzi ya Simba Kwa mujibu wa Ibara ya 11 (9) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, 2013, inatoa mamlaka kwa Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club kupeleka masuala ya maadili katika kamati ya maadili ya TFF. Tarehe 9 Juni 2014, Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club ilipeleka Masuala ya Maadili katika Kamati ya Maadili ya TFF. Kwakuwa TFF imekataa kusikiliza masuala ya maadili ambayo yanakiuka Kanuni za maadili, Katiba za Simba, TFF na FIFA, Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, itapeleka Masuala ya Maadili FIFA ili haki itendeke.

Pia kamati hiyo imesema kuwa uchaguzi wa simba uko palepale kwani wenye mamlaka ya kusimamisha uchaguzi wa simba no kamati ya uchaguzi na si vinginevyo.


" kamati ya uchaguzi ya simba ikichaguliwa inamamlaka ya kukaa miaka miwili pasipo kuingiliwa" alisema Ndumbalo


USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)


Post a Comment

0 Comments