Ticker

6/recent/ticker-posts

UBAGUZI WA RANGI:MWAMUZI WA MAN CITY LAZIMA AFUNGIWE

 Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA OKTOBA 24,2013 SAA 12:28 JIONI
Mwamuzi wa mechi ya Manchester City katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya CSKA Moscow hapaswi kuchezesha tena baada ya
kushindwa kukabiliana na unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi, amasema mwenyekiti wa chama cha kuzuia ubaguzi wa rangi katika soka nchini Uingereza Kick It Out, Lord Ouseley,.
Mchezaji wa City na kimataifa wa Ivory Coast alimlalamikia refa Ovidiu Hategan kuhusiana na ubaguzi kutoka kwa mashabiki CSKA wakati  wa mchezo wao siku ya jana.
Ouseley aliiambia BBC kwamba Hategan alikuwa "ameshindwa kufanya wajibu wake".
Hata hivyo, CSKA walisema "wameshangazwa nakukatishwa tamaa na madai ya Toure"

Lakinikatika hatua nyingine muungano wa wachezaji duniani wamekosoa uongozi wa soka  Ulaya UEFA kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake yenyewe juu ya ubaguzi wa rangi kufuatia unyanyasaji aliofanyiwaYaya Toure hapo jana
 "Niwazi  tumekatishwa tamaa sana kuona itifaki waliokubaliana ambayo iliyoundwa na kukabiliana na hali hii isiwezwe kutekelezwa," alisema Bobby Barnes, mkuu wa FIFPro's Europe division.
Sheria za mwaka 2009 za shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA ambazo zinatumika kuongoza mchezo huo zinampa mamlaka mwamuzi wa mchezo kushughulikia kejeli za ubaguzi wa rabgi kutoka kwa wafuasi.
Kwa hatua ya kwanza mchuano huweza kusimamishwa na kutoa onyo kwa watazamaji wote wanaofuatilia mchuano huo kwa wakati huo.
Hatua ya pili kwa mujibu wa sheria hiyo ni kuahirisha mchuano huo kwa muda mfupi ili kuona kama tabia hiyo imekoma ikiwa itaendelea hatimaye ni kufuta mchuano kabisa.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC mjini Moscow, Steve Rosenberg, anasema klabu ya CSKA Moscow inadai kwamba Toure peke yake ndiye alizisikia kelele hizo za ubaguzi wa rangi. 

Post a Comment

0 Comments