IMEWEKWA OCTOBA 16,2013 SAA 03:12 USIKU
![]() |
| Bruno Metsu |
Hivi karibuni tasnia ya michezo duniani imepata pigo kwa kupoteza wanamichezo watatu muhimu katika michezo mbali mbali, wa
kwanza ni Kocha raia wa Ufaransa Bruno Metsu anayefahamika zaidi kwa kuiongoza Senegal hadi katika robo fainali za kombe la dunia mwaka 2012, amefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Dunkirk kaskazini mwa France kutokana na ugongwa wa saratani akiwa na umri wa miaka 59.
Metsu aliliambia gazeti lilkip mwezi Julai mwaka huu kuwa amegunduliwa kuwa na kansa baada ya kufanyiwa uchunguzi na Daktari ambaye alitaka kufahamu ni sababu gani lizilosababibisha yeye kuugua mwishoni mwa mchezo wa mpira.
Bruno Metsu alistaafu kazi ya ukocha akiwa na klabu ya Al Wasl ya Dubai mwaka uliopita ili kupambana na ugonjwa wa saratani.
Evi bedelim ni mkurigenzi mtendaji wa klabu ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Ufaransa ambaye ni rafiki wa karibu wa Metsu amethibitisha taarifa hiyo na kusema amestushwa na taarifa hiyo.
Dereva wa mbio za magari Sean Edwards afariki katika ajali Australia
![]() | |||
| Sean Edwards dereva raia wa Uingereza ameaga dunia baada ya kupata ajali |
Dereva
wa mbio za magari ambaye anashiriki vema katika mchezo huo Sean Edwards
amefariki dunia katika mchezo huo baada ya kugongana huko Queensland
nchini Australia.
Muingereza huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 26
alikuwa ndani ya gari kama abiria wakati madereva wachanga walipokuwa
katika jaribio binafsi.
Edwards kwa siku za hivi karibuni ndiye amekuwa akiongoza ubingwa wa
mchezo huo awamu ambazo zinaenda sambamba na mbio za magari za Formula
1.
Edwards ambaye ni mtoto wa mwanamichezo wa siku nyingi alikuwa
akishiriki katika siku ya pili ya uangalizi kwa madereva wachanga huko
Queensland ambapo aliyekuwa akiendesha gari amejeruhiwa.
Kwa sasa kijana huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ambapo bado ana maumivu katika majeraha.
Dereva wa F1 Maria Villota afariki
![]() |
| Marie De Villota |
Dereva mashuhuri mwanamke wa mashindano ya langalanga
Formula 1 Maria De Villota amepatikana amefariki ndani ya chumba cha
hoteli moja mjini Seville,Hispania.
Msemaji wa polisi alisema."Tunachukulia kilikua
kifo cha kawaida,lakini hatuwezi kuthibitisha chochote na uchunguzi
utafanywa kuhusu kifo chake"
De Villota, mwenye umri wa miaka
33,alikua dereva wa akiba wa langalanga. Alipofuka jicho lake la kulia
katika ajali ya mwezi wa Julai mwaka jana alipokua akifanya mazoezi na
timu ya Marussia.
Alipata majeraha mabaya kichwani na usoni baada
ya kugongana na lorry katika jimbo la Cambridgeshire, Uingereza lakini
aliruhusiwa kuanza tena kuendesha gari.
Iliarifiwa De Villota, binti wa dereva wa zamani
wa mashindano ya Formula 1, Emilio De Villota,alikwenda Seville
kuzindua kitabu kuhusu maisha yake.
Timu na madereva wa langalanga wameelezea kushtushwa kwao na msiba huo.
Jenson Button wa Uingereza amesema.
"inasikitisha sana. Msichana huyu amekumbwa na masaibu mengi sana,
kupita yale yanayowakumba watu wengi duniani. Ni habari zilizotushtuwa
timu nzima na jamii nzima ya mbio za langalanga."
"tulimuona mwaka huu mjini Barcelona.Tukifanya
kazi kwa wakfu wa kuwasaidia watoto na alikua wa kwanza kujitolea na
kuwashawishi madereva wengi kujiunga nasi.Alikua akichangia mengi kwa
jamii ."



0 Comments