IMEWEKWA OCT. 8,2013 SAA 1:10 USIKU
Shirikisho
la soka nchini Ghana linaiomba shirikisho la soka duniani FIFA
kuhamisha mchuano wa marudiano wa kufuzu kwa kombe la
duniani nchini
Brazil dhidi ya Misri katika uwanja mwingine nje ya taifa la Misri kwa
sababu za kiusalama.
GFA kinasema kuwa kuna kinahofia usalama wa wachezaji wake
kutokana na visa vya uvunjifu wa amani ambavyo vimeendelea kushuhudiwa
katika nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, hasa baada ya watu 50
kuuawa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Cairo.
FIFA imepanga kuwa mchuano huo wa marudiano uchezwe tarehe 19 mwezi
Novemba jijini Cairo, mji ambao uongozi wa soka nchini Ghana unasema
kuwa hauna imani nao.
Mbali na kutokuwa na imani na mahali pa kuchezwa kwa mchuano huo,
chama cha soka nchini Ghana kinasema kuwa kinawahofia pia mashabiki wa
Misri ambao inaona wanaweza kuzua fujo uwanjani kama ilivyokuwa mwaka
uliopita wakati wa mchuano wa ligi kuu nchini humo na kusabisha vifo vya
zaidi ya mashabiki 70.
Ghana imeendelea kulalamika kuwa Misri imekuwa ikitumia uwanja wake
wa nyumbani kucheza mechi kadhaa za kufuzu kushiriki katika kombe la
dunia dhidi ya Msumbiji, Zimbabwe na Guinea bila ya mashabiki kufika
uwanjani kwa hofu ya mashabiki kupigana jambo ambalo pia inasema
linaweza kutokea.
FIFA inasema kuwa imepata ombi la Ghana na inafanya uchunguzi wake
kabla ya kutoa mwelekeo kuhusu ikiwa mchuano huo uondolewe jijini Cairo
au uendelee kuchezwa kama ilivopangwa.
Mchuano wa mzunguko wa kwanza wa kufuzu kwa kombe la dunia utachezwa mjini Kumasi tarehe 15 mwezi huu.

0 Comments