IMEWEKWA OCT. 18,2013 SAA 1:30 USIKU

Bruno Metsu wakati wa komne la dunia Qatar-Koweït à Doha
Heshima
za mwisho zimetolewa leo Ijumaa katika mji wa Dunkerque nchini Ufaransa
kwa mchezaji wa zamani na kocha
mfaransa Bruno Metsu aliefariki dunia
Octoba 15 akiwa na umri wa miaka 59, kabla ya kufanyika kwa mazishi
mwanzoni mwa juma lijalo nchini Senegal.

Mamia ya watu wakiwemo wachezaji wa zamani wa kimataifa wa timu
ya Senegal hususan Pape Diop na Hibi Beye pamoja na wachezaji wa zamani
wa kimataifa wa Ufaransa kama vile Roger Boli na Sabri Lamouchi ambao
walikuja kutowa heshima zao za mwisho kwa kocha huyo wa zamani wa timu
ya taifa ya Senegal aliefaulu kuifikisha timu iyo kwenye ngazi ya robo
fainali katika kombe la dunia mwaka 2002.
Balozi wa Senegal nchini Ufaransa Paul Badji, katika hotuba yake fupi amewapongeza wale wote waliojitokeza kumuaga kwa mara ya mwisho kocha huyo ambaye Senegal inataka kumfanya kuwa kinara. Akiambatana na seneta wa jiji la Dunkerque Michel Delebarre pamoja na kiongozi wa zamani wa kalbu ya Marseille Pape Diouf pamoja na rafiki wa karibu na Marehemu Bruno Metsu Alex Dupont kocha wa klabu ya Brest.
Shughuli hizo zimefanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa USL Dunkerque ambako Bruno Metsu aliutumia kwa kucheza na hata mara kdhaa bila viato.
Mke wa Marehemu na dada yake Viviane na veronique walipishana katika kutowa ushuhuda wao kuhusu mpendwa wao na jinsi gani walivyomsaidia kupambana na maradhi.
Balozi wa Senegal nchini Ufransa Paul Badji amesema Mwili wa Marehemu Metsu utasafirishwa katika siku za usoni nchini Senegal ambako atafanyiwa mazishi ya kitaifa, ambaye alifahamisha kuwa Bruno Metsu alikuwa ni miongoni mwa raia wa Senegal, hivo aliamuwa kueshi nchini Senegal na kutowa mafunzo kwa mchezo ambao unaopendwa na raia wa Senegal.
Shughuli za kidini ambazo zilikuwa zimepangwa kufanyika katika kanisa la Saint Eloi ya Dunkerque hazikufanyika kufuatia vile Bruno Metsu alikuwa tayari ameslimu na kuwa Muislam.
Veronique Dada wa Marehemu, amesema Senegal ilikuwa ni nchi yake anayo ipenda ni jambo la kawaida sana kuzikwa nchini humo.
Kabla ya kuwa kocha Bruno Metsu alikuwa mchezaji katika daraja la kwanza nchini Ufaransa, na alizichezea Valanciennes, Lille na Nice. Na aliwahi kuw akocha wa vilabu vya Lille, Valenciennes, Bauvais na Sedan nchini Ufaransa. Alijulikna sana baranai Afrika baada ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya Guinea, na Senegal barani Afrika, kabla ya kuelekea barani Ashia Saudi arabia na Qatar.
CHANZO:rfi kiswahili

0 Comments