Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA OKTOBA 27,2013 SAA 02: 24 USIKU
Carlo
Ancelotti aliona Real Madrid wanapaswa kupewa penarti wakati timu yake ilipofungwa 2-1 na Barcelona katika Uwanja wa
Nou Camp.
Mabao kutoka kwa Neymar na Alexis Sanchez yaliiwezesha Barcelona kuondoka na pointi 3 muhimu,licha ya bao la kutiafaraja kwa upande wa Real kupitia kwa Jesé Rodríguez..
Hata
hivyo, Ancelotti alililamikia changamoto aliyofanya Javier Mascherano juu ya
Cristiano Ronaldo katika dakika 19 wakati Barcelona wanaongoza 1-0, anasema Real ilistahili kupata penalti.
Mwamuzi
Alberto Undiano Mallenco hakusitisha mchezo kuchezwa baada ya Ronaldo kuanguka
chini kwa changamoto ya muargentina huyo, ili Ancelotti amewasilisha hasira za timu yake ya
Real Madrid.
"Ki ukweli penalti ilikuwa wazi sana kwa upande wangu mimi,nafikiri kila
mtu aliona hayo, mtu ambaye hakuweza kuona ilikuwa ni mwamuzi,"
Ancelotti alisema katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi.
![]() |
| Cristiano Ronaldo akililia penalt. |
Wachezaji Real walidhani wangeweza kuzawadiwa kupiga mpira wa adhabu kuelekea mwisho
wa nusu ya kwanza,kwa kuwa mpira uligusa mikono wa mchezaji wa Barca Adriano.
MBrazil huyo tayari alikuwa na KADI ya kabla ya tukio hilo na Ancelotti akasema"Ni uamuzi
mgumu, lakini ilikuwa ni wakati muhimu kama adhabu ingetolewa na angeweza kutoa hata kadi nyiingine ya njano pia"



0 Comments