Ticker

6/recent/ticker-posts

MH.MAGUFULI KUONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI NZIMA YA WAHANDISI YATAKAYOANZA JUMAPILI

Na. Herman Kihwili.IMEWEKWA SEPT. 19,2013 SAA 6:50 MCHANA
 
Eng. Dkt. Malima M.P. Bundara RAIS WA TAASISI YA WAHANDISI TANZANIA

Kila mwaka tangu 2012, TAASISI YA WAHANDISI TANZANIA inatayarisha na kuratibu maadhimisho ya Wiki ya Wahandisi. Maadhimisho haya hufanyika kote nchini kwa wahandisi pamoja na
mafundi kufanya kazi za kujitolea wakishirikiana na wanachi.
1.     Lengo la maadhimisho haya lina sura mbili muhimu.
Ø Kuukumbusha umma na watanzania umuhimu wa uhandisi katika maendelo ya Taifa letu. Hakuna nchi yoyote inayoweza kupata mandeleo bila kuwepo kwa wahandisi.
Ø Kuwaomba na kuwahamasisha watanzania kutumia kila aina ya mbinu kujenga na kuendeleza uwezo wa wahandisi watanzania (Local engineers).

2.     Maadhimisho haya huzinduliwa kwa Matembezi ya Hisani (Charity Walk) yenye madhumuni ya kukusanya fedha zitakazotumika kutekeleza mradi kabambe wa kujenga uwezo wa wahandisi wetu unaendelea kutekelezwa na Taasisi ya Wahandisi. Ingawa mradi huu unatakelezwa kwa awamu ya miaka minne minne, unatakiwa kuwa endelevu. Tunategemea kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014, wahandisi wote wahitimu (fresh graduates) watakuwa wanaingia moja kwa moja kazini kupata mafunzo ya kazi (internship). Hivi sasa wahandisi wahitimu wanaachwa bila kazi wakati mahitaji ya wahandisi nchini ni makubwa, kupita kiasi.

3.     Maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika kama ifuatavyo ;
Ø  Jumapili tarehe 22/09/2013 kutakuwa na Matembezi ya Hisani (Charity Walk) ya wahandisi wote pamoja na familia na marafiki zao. Mgeni Rasmi katika matembezi hayo hapa Dar es Salaam anategemewa kuwa Waziri wa Ujenzi, Mhe. Dkt. John P. Magufuli (Mb) Matembezi yataanzia ofisi za Taasisi na kuishia kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni. Wahandisi wa huko mikoani wamepanga ratiba zao.

Ø  Jumatatu hadi Ijumaa wahandisi kote nchini watajishughulisha na kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea shule mbalimbali kuhamasisha na kufundisha masomo ya sayansi.

Ø  Siku ya Ijumaa maadhimisho yatahitimishwa kwa kushiriki kwenye Chakukula cha Usiku cha kila mwaka (Annual Dinner). Mgeni rasmi kwenye chakula hicho hapa Dar es Salaam atakuwa Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji na uwezeshaji) Mhe. Dkt. Mary Nagu (MB). Tukio hili litafanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

4.     Taasisi ya Wahandisi Tanzania inaomba kama ifuatavyo ;
Ø Watanzania na hasa wahandisi na mafundi wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye maadhimisho haya. Inafaa kukumbuka kwamba matatizo na misuguano inayoisumbua nchi yetu sasa inatokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na ; ukosefu wa ajira, uhaba wa chakula, maji, nishati, miundombinu na mengine mengi. Matatizo haya hayawezi kumalizwa kwa mikutano ya hadhara na kulalamika. Lazima tufanye kazi na hasa kwa kuwatumia wahandisi wetu wa ndani. Utegemezi kwa wahisani hautatusaidia. Tuwaite wahisani kuongoza nguvu siyo kuongoza mapambano.

Ø Waandishi wa habari wachukue hatua za makusudi kuandika mambo yanayofanyika kutatua matatizo ya nchi baada ya kujikita zaidi kuandika matatizo na matukio yanayotokana na matatizo hayo. Kuendelea kufanya hivyo ni kuzidisha hamasa za uhalifu na kuwakatisha tamaa watanzania wenye nia ya kuendeleza taifa hili.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
 

Post a Comment

0 Comments