Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA:GARETH BALE ATOSWA KUANZA KATIKA MECHI DHIDI YA SERBIA

 Mhariri:Herman Kihwili,IMEWEKWA SEPT 10,2013 SAA 6:20 USIKU
Licha ya Gareth Bale kuwa katika mazoezi na timu yake ya taifa ya  Wales lakini,imethibitishwa kuwa,hataanza kucheza  katika mechi ya kuwania kufuzu kombe la  Dunia siku ya leo  dhidi ya Serbia.

Mchezaji huyo mpya wa Real Madrid aliyesainiwa kwa £ 86m ambaye alikuwa akishuhudia kipigo akiwa katika benchi siku ya 
Ijumaa iliyopita wakati timu yake ilipofungwa 2-1 dhidi ya Macedonia, na kusababisha hasira kutoka baadhi ya mashabiki wa Wales.
Chris Coleman:"Haitawezekana Bale kuanza siku ya Jumanne"
Meneja Chris Coleman alisisitiza nyota  huyo alijeruhiwa, na aliyasema hayo  wakati  alpoulizwa maswali juu ya uteuzi wake wa kikosi. 
Akizungumza mapema na  Sky Sports News, Coleman alisema: "Pamoja na yeye kutocheza michezo yeyote,lakini pia hakutawezekana kuanza siku ya Jumanne(leo),  kamwe" 
"ikiwa  ameshapata mafunzo kwa vipindi  vitatu hadi vinne,mara  sita hadi nane kwa wiki, ni vizuri kama yeye,lakini  anaweza kuwa hatarisha wachezaji."  

Post a Comment

0 Comments