Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII NA MICHEZO YAWA MSHINDI WA PILI

 IMEWEKWA SEPT. 22,2013 SAA 9:32 USIKU
Hatimaye lile shindano la Tanzania Bloggers Awards limemalizika rasmi siku ya jana jumamosi ya tarehe 21 mwaka 2013,na kama ulivyokuwa ufahamu blog ya Jamii na Mchezo pia ilikuwa ni moja ya blog zilizoshiliki katika shindano hilo,hakika Jamii na Michezo inatambua nia ya kuipigia kura blog hii ni kutaka iwe ya kwanza katika kipengele cha The Best Sports Blog.
Lakini kama unavyofahamu haya ni mashindano kuna kuzidiana kura zinazopigwa,na blog ya Jamii na Maichezo katika kipengele cha The Best Sports Blog ilikuwa inashindana na blog takribani 7,lakini kwa nguvu ya kura uliyoipiga,umeifanikisha kuwa mshindi wa pili.
Hii inaonesha jinsi gani kura uliyopiga haija potea,basi blog hii inatumia nafasi hii kukushukuru wewe uliyepiga kura kuichagua Jamii na Michezo iwe The Best Sports Blog,na hakika sasa inatambua kuwa haiko peke yake bali pia na ndugu yake ambaye ndio wewe msomaji.
Jamii na Michezo rasmi ilianza kupeperu habari zake ilikuwa siku ya jumatatu ya tarehe 12 mwezi wa 8 mwaka huu 2013,mpaka hapo utaona jini gani ni muda mchache wenye mafanikio ya wasomaji,.
Jamii na Michezo inachukua nafasi hii kukuahidi msomaji wa blog hii kwamba haita kuangusha hata kidogo,bali kuendelea kukuleta taharifa za ukweli na zilizokuwa katika wakati kwani kazi ya Jamii na Michezo ni kukuhabarisha,kukuelimisha na kukuburudisha pia.
Tuendelee kushilikiana kwa wakati wote kama ilivyo sasa,na kama unatumia mtandao wa kijamii wa facebook basi usisahau ku-like ukurasa wako wa Jamii na michezo, na katika google pi kama ukitafuta Jamii na Michezo,basi usiache nafasi yaani (jamiinamichezo).

Mungu ndiye muweza wa yote,sifa na utukufu ziende kwake.

Team Jamii na Michezo:Herman Kihwili pamoja na wewe msomaji.

        Kwa pamoja tutaweza na tutafika.
 Asante kwa clesensia Kihwili pamoja na Team GK;Elie,Ambwene pamoja na Silas.

Mhariri/Mkurugenzi/mwandishi:Herman Kihwili

 Kwa maoni na kama una taharifa:hermankihwili@gmail.com
  Simu No.  0659274594
Facebook: Herman Kihwili
Twitter:Herman Kihwili
             
 

Post a Comment

0 Comments