Ticker

6/recent/ticker-posts

EVERTON 3 NEWCASTLE 2:LUKAKU AONGOZA MAHANGAMIZI WAKIWA NYUMBANI

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA SEPT 30,2013 SAA 08:13 USIKU
 Mtu mkuu: Romelu Lukaku alifunga mabao mawili ya Everton na kuipa  Newcastle wakati mgumu katika Uwanja wa Goodison Park
Michezaji wa Everton  Romelu Lukaku ameisaidia timu  yake kuibuka na ushindi wakiwa nyumbani baada ya kupachika mabao
mawili peke yake katika  ushindi wa 3-2 katika Uwanja wa Goodison Park siku ya Jumatatu dhidi ya timu ya Newcastle United.
Alifungua mchezo kwa kufunga: Lukaku alihitaji dakika tano tu kuipatia bao la kwanza Everton 
Mkali cheche: Ross Barkley iliendelea kuonyesha uwezo wake kwa kufunga bao la pili kwa Everton
Machozi kabla ya kwenda kulala: Dogo shabiki wa  Newcastle  alionekana kutokuwa na  furaha baada ya kufungwa na Everton
Goli la Wazi : kosa kwa wachezaji wa  Newcastle kumruhusiwa Lukaku kushinda na akiumiliki mpira

Evarton walionesha kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza kwa kupiga mabao yote matatu ndani ya kipindi hiko.Na bao la kwanza lilipatikana katika dakika ya 5 kupitia kwa Romelu Lukaku,na baada ya dakika ishirini Ross Barkley akipokea pasi ya Lukaku akaiandikia Everton bao la 2,kisha Romelu Lukaku tena akafunga ukurasa wa mabao wa Everton katika dakika ya 37 kwa kuizawadia timu hiyo bao la tatu.
Bao safi: Yohan Cabaye alipiga mpira kutoka nje ya boksi na kuweza kushinda bao la kwanza na kutoa matumaini kwa  Newcastle
Newcastle walikuwa dhaifu katika nusu ya kwanza lakini walizinduka na kushinda baada ya kuanza kipindi cha pili ndani ya dakika ya 51 Yohan Cabaye alipachika bao la kwanza (nje ya Box) kwa upande wa Newcastle na faraja ikazidi kuongezeka kwa timu hiyo baada ya  kupata bao la pili kupitia kwa  Loic Remy katika dakika ya 89. Kiukweli walionekana wanauchu wa kusawazisha katika dakika nne  zilizoongezwa lakini mpaka muda unakamilika waliambulia kubaki na mabao hayo hayo mawili kwa matatu ya Everton.
Tunatafakari mengi:Mmiliki wa  Newcastle  Mike Ashley (kushoto) na Joe Kinnear  wakiangalia jinsi timu yao inavyosurubishwa
                  VIDEO YA MAGOLI YOTE
                                     
BADGESKIKOSI CHA EVERTON (4-4-1-1) Howard 6; Baines 7, Distin 7, Jagielka 7, Coleman 7; Mirallas 8 (Deulofeu 73, 6), McCarthy 7, Barry 8, Osman 7 (Stones 90); Barkley 8 (Naismith 88); Lukaku 9

Akiba wasiotumika: Robles, Heitinga, Jelavic, Kone.
Wafungaji: Lukaku 5, 37, Barkley 25.
Kadi za njano: Baines, Mirallas, Barry.

BADGES
KIKOSI CHA NEWCASTLE UNITED: (4-3-3): Krul 5; Debuchy 5, Yanga-Mbiwa 4 (Williamson 45, 6), Coloccini 4, Santon 4; Anita 5 (Cisse 69, 5), Tiote 5, Sissoko 5; Gouffran 6, Remy 6, Ben Arfa 5 (Cabaye 45, 7)
Akiba wasiotumika : Elliot, Obertan, Sammy Ameobi, Dummett.
Wafungaji: Cabaye 51, Remy 89.
Kadi ya njano: Tiote.

Post a Comment

0 Comments